Bwiza
ads

APR FC Yaagana na Wachezaji 6, Wakiwemo Wageni 4

Michezo•
Fred Karege
By Fred Karege
•Kuwa Gatandatu, 14 Kamena 2025 saa 14:46
Iminota 1 yo gusoma
APR FC Yaagana na Wachezaji 6, Wakiwemo Wageni 4

Klabu ya APR FC imethibitisha kuwa imeagana na wachezaji sita, wakiwemo wachezaji wanne wa kigeni.

Klabu hiyo imeachana nao baada ya mikata yao kumalizika rasmi.

Wachezaji waliotajwa kuondoka ni Taddeo Lwanga (Uganda), Victor Mbaoma (Nigeria), Pavelh Ndzila (DRC), Nshimirimana Ismaël (Burundi), na Warwanda wawili: Kwitonda Alain na Ndayishimiye Dieudonné.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa X, APR FC iliwaambia:

“Asanteni sana kwa muda mzuri tuliokuwa pamoja, na tunawatakia kila la heri katika maisha yenu mapya.”

Ripoti zinaeleza kuwa APR FC imekwisha sajili wachezaji wapya kuchukua nafasi zao, akiwemo Ronald Sekiganda kutoka Uganda, na Warwanda Iraguha Hadji na Bugingo Hakim, ingawa klabu haijathibitisha rasmi taarifa hizi.

Fred Karege

Inkuru yanditswe na: Fred Karege

Umunyamakuru wa BWIZA.COM wanditse inkuru 2,508.